ACHANA NA ‘SIWEZI KUISHI BILA YEYE’, KUNA MAISHA BILA YEYE !

HAKUNA shaka tulio wengi tupo katika uhusiano wa kimapenzi wa mashaka. Hakuna hata mmoja wetu ambaye anaweza kujiaminisha kwa asilimia mia moja kwamba mpenzi wake aliye naye anampenda kwa dhati kabisa au anazuga. Hii inabaki kuwa siri ya anayependa!

Lakini sasa, kuna kitu nilichogundua miongoni mwetu, kitu ambacho tusipokuwa makini nacho tunaweza kujikuta tunajilazimisha kuishi maisha ya huzuni wakati tunayo haki ya kuishi maisha ya yenye furaha. Ukweli ni kwamba, kila mtu anao uhuru wa kupenda kwani maisha bila mapenzi lazima yatakuwa na kasoro.

Lakini sasa, uhuru huo usikufanye ukalazimika kumpenda mtu ambaye anaonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya dhati kwako. Waswahili wanasema, mpende akupendaye, asiyekupenda achana naye. Huo ndio ukweli wenyewe hasa linapoingia suala la mapenzi. Hivi utampendaje mtu ambaye hakupendi? Sawa, huwezi kujua kwamba hakupendi kwani huwezi kuufungua moyo wake lakini, kuna dalili za wazi zinazoweza kukudhihirishia kuwa, mtu huyo anakuzingua tu na kutaka kukupotezea muda wako.

Kitu kinachoniuma na ambacho ndicho kimenisukuma kuandika makala haya ni tabia ya baadhi ya watu kung’ang’ania wapenzi ambao wanaonesha kabisa kutowapenda, ukimuuliza kwa nini anamng’ang’ania wakati hapati anachokitaka, anakuambia eti anampenda sana. Jamani ifike wakati tutambue kuwa, kutokea kumpenda mtu na yeye akakupenda kwa dhati ni bahati sana. Wengi wetu tunatokea kuwapenda watu wasiotupenda, matokeo yake ni kuumizwa kila wakati.

Wewe jaribu kuchunguza utabaini walio wengi hawapati mapenzi wanayoyatarajia kutoka kwa wapenzi wao badala yake huishia kilizwa kila mara. Niseme tu kwamba, kanuni ya mapenzi inasema, nipe nikupe, nipende nikupende, niheshimu nikuheshimu. Kama unabaini dalili f’lani f’lani za wazi kwamba mpenzi wako hakupendi usijilazimishe kuendelea kumpenda. Ukifanya hivyo utamfanya aendelee kukunyanyasa.

KIPI CHA KUFANYA?


Huenda wewe unayesoma makala haya sasa hivi ukawa unajiamini sana kwamba mpenzi wako anakupenda, hiyo ni nzuri na ndivyo ambavyo kila mtu anatakiwa kuishi. Tambua ukiwa na imani kwamba mpenzi wako anakupenda itakufanya uishi maisha ya furaha na amani huku na wewe ukijitahidi kuonesha kumpenda kwa dhati, hapo mtaishi.

Lakini kama unaona penzi la mpenzi wako ni la mashaka ni wakati wako wa kuamini kwamba, unaweza kuishi hata yeye  asipokuwepo. Kauli ya ‘siwezi kuishi bila yeye’ imepitwa na wanaoishi kwenye dhana hiyo ni malimbukeni. Bila yeye huwezi kuishi kwani yeye amekuwa hewa ya oksijeni?

Hee! Aende zake kama anaona wewe huna hadhi ya kuwa naye lakini akae akijua kwamba, penzi analolipiga teke wapo ambao wanalitafuta na hawalipati. Kwa nini ujizibie bahati yako kwa kumng’ang’ania mtu ambaye moyo wako umemtapika? Jamani hakuna anayeshikilia pumzi ya mwingine, akikuacha huyo uliye naye maisha yako yatayumba kwa muda tu kisha utampata mwingine na maisha yako yataendelea wala hutakufa kama baadhi wanavyofikiria!

Kuendelea kumpa nafasi ni kujipa presha na vidonda vya tumbo bure, magonjwa ambayo ndiyo yanaweza kukutoa duniani na si kwa kumuacha huyo. Kumbuka, ni wewe na maisha yako! Maamuzi yako ndiyo yatakufanya uishi kwa furaha au amani. Upo ndugu yangu?
Name

Afya Magazeti Makala Mapenzi Matukio Michezo News Siasa Udaku Urembo Wasanii
false
ltr
item
www.yanayojiri.com: ACHANA NA ‘SIWEZI KUISHI BILA YEYE’, KUNA MAISHA BILA YEYE !
ACHANA NA ‘SIWEZI KUISHI BILA YEYE’, KUNA MAISHA BILA YEYE !
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjCmTobGEDKLg6OQrChuSz2PN8muj7Ilu_wL8cqe_e0_CKyBU8IiFMIXYgP3TGbNDngTiGx6vRd_gVSNv4lv0CaNpKbfb6PpKI192V1AQPvcMkpGdExE_1UsvrZabBf8egoLGWVWm6sW44/s640/Romantic-Ways-To-Give-Birthday-Surprise-To-Your-Wife.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjCmTobGEDKLg6OQrChuSz2PN8muj7Ilu_wL8cqe_e0_CKyBU8IiFMIXYgP3TGbNDngTiGx6vRd_gVSNv4lv0CaNpKbfb6PpKI192V1AQPvcMkpGdExE_1UsvrZabBf8egoLGWVWm6sW44/s72-c/Romantic-Ways-To-Give-Birthday-Surprise-To-Your-Wife.jpg
www.yanayojiri.com
http://nipasheapp.blogspot.com/2018/10/achana-na-siwezi-kuishi-bila-yeye-kuna_9.html
http://nipasheapp.blogspot.com/
http://nipasheapp.blogspot.com/
http://nipasheapp.blogspot.com/2018/10/achana-na-siwezi-kuishi-bila-yeye-kuna_9.html
true
3144336648072757917
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy
© Copyright www.yanayojiri.com | Designed By Me