
Alipohitimu alikwenda kufanya kazi na Wall Street lakini mwaka 1994 aliacha kazi na kwenda kuanzisha Amazon, ambapo kwa mara ya kwanza Amazon ilianzishiwa katika karakana ya kutengenezea magari. Baada ya kampuni hiyo kuanza kufanikiwa na kujipanua katika nchi mbalimbali, mwaka 2000 alianzisha kampuni ya Blue Origin inayojishughulisha na masuala ya anga.
Kwa miaka ya hivi karibuni amekuwa akijikita zaidi katika mradi wake wa Blue Origin unaohusika na urushaji wa rocket kwenda angani pamoja na Washington Post ambazo zote anazimiliki.
Mwaka 2013 akiendelea kujipanua, aliinunua Kampuni ya Washington Post kwa $250 milioni na ilipofika julai 2017 alitajwa kuwa dola za kimarekani 90.6 bilioni.
Mpaka sasa amefikisha utajiri wa dola za kimarekani bilioni 105.1 na anakisiwa kuwa atakuwa ndiye trilionea wa kwanza duniani.
Amemuoa mwandishi wa vitabu, Mackenzie Bezos na wana watoto wanne.