Ufahamu utaratibu wa kufuata ili kupata cheti cha kuzaliwa

Usajili wa vizazi unasimamiwa na sheria ya uandikishaji vizazi na vifo,(sura 108 toleo la 2002)

Kulingana na sheria kizazi inatakiwa kuandikishwa ndani ya siku 90 tangu kutokea kwake na kifo ndani ya siku30,na Tukio hilo Lazima liwe limetokea ndani ya mipaka ya Tanzania Bara.Pamoja na takwa hili sheria inaruhusu usajili kufanyika nje ya muda huu.Wajibu wa kusajili kizazi ni kama ufuatao:

NB: Baba au Mama,na kama Baba na Mama hawapo,mmiliki wa nyumba ambaye ana taarifa za kizazi kutokea,mtu yoyote ambaye amekuwapo wakati kizazi kikitokea au mtu yoyote ambaye mtoto aliyezaliwa yuko katika himaya yake.

UTARATIBU WA KUPATA CHETI CHA KUZALIWA


1: Usajili wa kizazi ndani ya siku 90


    Kama kizazi kimetokea hospitalini,kituo cha afya au zahanati hakikisha unapatiwa Tangazo la kizazi kabla ya kuondoka.
    Endapo kizazi kitakuwa kimetokea nyumbani,toa taarifa kwa Afisa Mtendaji wa kijiji au Msajili wa kizazi au vifo wa wilaya ili ipatiwe tanzazo la kizazi.taarifa hii itolewe ndani ya siku 90.
    Wasilisha tangazo la kizazi kwa msajili wa kizazi na vifo wa wilaya kilipotokea kizazi
    Lipa ada ya cheti inayotozwa (ada ya sasa ni shilingi 3500/=).

2: Usajili nje ya siku 90 lakini chini ya miaka 10.


    Jaza na wasilisha fomu BD15 (ijazwe na mzazi au mlezi)
    Bandika picha ya mtoto(passport size)ambaye kizazi chake kimeombewa kusajiliwa.
    Ambatanisha nyaraka za kuunga mkono maelezo yako kwenye fomu.nyaraka hizi ni :-passipoti, cheti cha kumaliza elimu ya msingi, sekondari, kadi ya kliniki,cheti cha ubatizo(kama unahusika),barua kutoka ofisi za serikali zinazohusika kama ofisi ya mtendaji wa kata;mtendaji wa kijiji.
    Lipia ada inayotozwa (ada ya sasa ni shilingi 4000/=)

3: Kuandikisha kizazi kilichochelewa kuandikishwa zaidi ya miaka 10


    Jaza na wasilisha fomu BD15 (ijazwe na mzazi au mlezi).
    Bandika picha ya mtoto(passport size)ambaye kizazi chake kimeombewa kusajiliwa.
    Ambatanisha nyaraka ,kadi ya kliniki ya mtoto,cheti cha ubatizo kamakipo,barua kutoka mamlaka ya serikali zinazohusika kama vile ofisi ya mtendaji kata au kijiji),cheti cha kuthibitisha tarehe ya kuzaliwa,mahali pa kuzaliwa na uraia wa wazazi.
    Lipa ada inayotozwa (ada ya sasa ni Tshs 10,000/=).

4: Kupata makala ya cheti baada ya kupoteza .


    Wasilisha ombi lako ukionyesha namba ya ingizo ,jina la mwenye cheti,mahali pa kuzaliwa na tarehe ya kusajiliwa.
    Lipa ada inayotozwa (ada ya sasa ni Tsh.3500/= ikiwa Tshs.1500/= ada ya upekuzi na Tsh 2000/= ada ya makala ya cheti.

5: Kufanya masahihisho kwenye cheti cha kuzaliwa


    Kufanya masahihisho kwenye cheti cha kuzaliwa
    Ambatanisha nyaraka za kuunga mkono ombi lako – barua inayotetea ombi lako na kiambatanisho(kitambulisho cha kura n.k)
    Rejesha cheti kinachotakiwa kusahihishwa.
    Ada baada ya ombi lako kukubaliwa (ada ya sasa ni Tsh6500/=(ikiwa ni:-3000/= ada ya kusahihisha , 1500/= ada ya upekuzi na 2000/= ada ya cheti)

Utaratibu wa Kupata Cheti cha Kuzaliwa, kwa Watu Walio Nje ya Nchi.

Hatua ya Kwanza:


    Tuma barua pepe ya maombi kupitia info@rita.go.tz
    Ambatanisha na kimojawapo kati ya viambatanishi vifuatavyo (Clinic card, Cheti cha ubatizo, School leaving certificates [Shule ya msingi, Sekondari]), kwa uhakika wa tarehe ya kuzaliwa mtoto, sehemu ya uzaliwa na uraia wa wazazi.
    Pakuwa fomu BD15 (kwa Usajili wa mtoto zaidi ya siku 90, lakini chini ya miaka 10), au fomu BD15(kwa Usajili wa mtoto zaidi ya miaka 10). Jaza na zitume kwa barua pepe info@rita.go.tz
    Fomu za kupakuwa zinapatikana hapaHatua ya Pili:
    Utapokea barua pepe kutoka RITA, iliyoambatanishwa na fomu ya Afidavit, kutoka kwa Msajili Mkuu.
    Printi na jaza fomu ya Afidavit, kisha iambatanishe na picha 3 za passport size.
    Scan fomu ya Afidavit, itume kwa barua pepe kuelekea info@rita.go.tzHatua ya Tatu:
    Utapokea barua pepe kutoka RITA, ikikupa ruhusa ya kulipia.
    Malipo ya kusafirisha cheti yatategemea huduma utakayoamua kutumia (DHL, EMS n.k)Malipo:
    Cheti cha mtoto chini ya miaka 10 – $14.
    Cheti cha mtoto zaidi ya miaka 10 – $20.
    ku-clear cheque – $20.Tanbihi:
    Utatakiwa ufanye uchunguzi ili kufahamu Malipo ya kusafirisha Cheti ni bei gani, halafu utume fedha (ya kulipia cheti), pamoja na fedha ya kukombolea mzigo(fedha).
    Tunasisitiza malipo kwa fedha taslimu.
Name

Afya Magazeti Makala Mapenzi Matukio Michezo News Siasa Udaku Urembo Wasanii
false
ltr
item
www.yanayojiri.com: Ufahamu utaratibu wa kufuata ili kupata cheti cha kuzaliwa
Ufahamu utaratibu wa kufuata ili kupata cheti cha kuzaliwa
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgWdrTSVlPD8pZdPXhIicI23Z7N_noja55ePgpLD-9qOEO-b3QaN_8Imgyt9S2yN_L9e0dazcXAm5t7rOfQUHBffjpQJCnyMwtlNQ6pDYejhCwcm8Z8itWmWkzvxl_181aDzx4qftwkedM/s640/birth_certificate.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgWdrTSVlPD8pZdPXhIicI23Z7N_noja55ePgpLD-9qOEO-b3QaN_8Imgyt9S2yN_L9e0dazcXAm5t7rOfQUHBffjpQJCnyMwtlNQ6pDYejhCwcm8Z8itWmWkzvxl_181aDzx4qftwkedM/s72-c/birth_certificate.png
www.yanayojiri.com
http://nipasheapp.blogspot.com/2018/10/ufahamu-utaratibu-wa-kufuata-ili-kupata.html
http://nipasheapp.blogspot.com/
http://nipasheapp.blogspot.com/
http://nipasheapp.blogspot.com/2018/10/ufahamu-utaratibu-wa-kufuata-ili-kupata.html
true
3144336648072757917
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy
© Copyright www.yanayojiri.com | Designed By Me