Fahamu mpangilio wa gia kwenye gari ya ‘manual transmission’ na namna ya kuzitumia

Katika Makala zilizopita tulizungumzia mambo ambayo hupaswi kuyafanya unapoendesha gari la ‘manual transmission’.

Katika uendeshaji wa gari la ‘manual transmission’ huwa inahusisha dereva kubadili gia kulingana kadiri gari linavyozidi kutembea ili kuufikia mwendokasi anaoutaka. Tofauti kubwa iliyopo kati ya gari la ‘Manual transmission’ na lile la ‘automatic transmission’ huwa ni utendaji wa gearbox. Gearbox ya manual inamtaka dereva wa gari husika kubadili gia kila mara ili apate mwendokasi pamoja na spidi inayohitajika kwa wakati huo kutegemeana na kiwango cha mzigo kilichopo kwenye gari, hali ya barabara, mwinuko wa barabara pamoja na mwendokasi.

Kwa gari za ‘automatic’ dereva atahitajika kuweka gia ‘D’ kwa maana ya drive ili gari lisonge mbele ambapo mpangilio wa gia utabadilika wenyewe kulingana na kiwango cha mafuta alichokiruhusu dereva kuingia kwenye injini pamoja na hali ya mwinuko au utambarare wa barabara.

Gearbox ni kifaa kilichopo katika gari ambacho ndani yake kuna mkusanyiko wa gia zinazotofautiana ukubwa, na hata uwezo wa kuzunguka na kulipa gari nguvu pamoja na mwendokasi.

Leo tutaangalia sana namna ya utumiaji gia kwenye gari lenye mpangilio wa gia 6, yaani tano za mbele na moja ya nyuma (R).  Japo hata kwa gari zenye gia 7 (1,2,3,4,5,6, R) namna ya utumiaji wake ni sawa na gari yenye gia 6.

Ni kawaida kabisa kwa dereva yeyote anapoondoa gari huanza na gia namba moja. hii ni kwa sababu gia hii ina nguvu kubwa sana kuliko gia nyingine zote katika gari. Gia namba moja mara nyingi hutumika wakati gari linapoondoka, linapokuwa katika mwendokasi chini ya 10 kph, linapokuwa linapanda mlima mrefu na mkubwa nk. sito kwa maeneo haya tu ambapo gia namba moja inatumika yapo mengine ambayo unaweza ukawa unayajua lakini hatujayataja. usisite kushare nasi katika comment section hapo chini.

Gia namba moja huwa inatumia kiasi kikubwa cha mafuta ili iweze kupata nguvu ya kuliwezesha gari kuondoka. Unashauriwa kuitumia pale tu ambapo kuna ulazima ili kuokoa kiwango cha mafuta ambacho utakitumia katika safari yako.

Gia namba mbili nayo ina nguvu lakini siyo kama namba moja. Nayo hutumika katika maeneo kama kupanda mlima lakini inaposhindwa kuendelea ndipo namba moja huchukua nafasi yake. Kwa gia namba 2 mwendokasi huongeseka kidogo na kiwango cha mafuta kinachotumika hupungua ukilinganisha na kile kinachotumiwa na namba moja.

Kwa gia namba 3, 4 na 5 ulaji wake wa mafuta unapungua kadiri unavyoongeza gia lakini pia mwendo unaongezeka. ga hizi hutumika katika maeneo yasiyo na miinuko na wakati gari liko katika mwendo wa zaidi ya zaidi ya 30 kph ili iweze kuwa na nguvu iliyotakiwa. ukiweka gia hiyo ukiwa chini ya mwendokasi huo gari inaweza ikazima.

Kwa gia ya ‘reverse’ hi  hutumika kulirudisha gari gari nyuma. Gia hii nayo ina nguvu sana kwani iko peke yake japo kwa baadhi ya magari huwa na gia zaidi ya moja ya ‘reverse’.
Name

Afya Magazeti Makala Mapenzi Matukio Michezo News Siasa Udaku Urembo Wasanii
false
ltr
item
www.yanayojiri.com: Fahamu mpangilio wa gia kwenye gari ya ‘manual transmission’ na namna ya kuzitumia
Fahamu mpangilio wa gia kwenye gari ya ‘manual transmission’ na namna ya kuzitumia
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEisBBIlrk9IIIIjgDtT2dFUCTIY4Vpp4en8nS1COkQn-yevyMYAz1ZMr3cuR6LqJ-TcNDf4Ds5HFZHKQUB-4VmXna5yu_Q_9GtEbaCLBnUQ0W70OXsMPAnjthqNEPRwHjrSuunSdWEYpkc/s640/rsz_2373334_l-750x375.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEisBBIlrk9IIIIjgDtT2dFUCTIY4Vpp4en8nS1COkQn-yevyMYAz1ZMr3cuR6LqJ-TcNDf4Ds5HFZHKQUB-4VmXna5yu_Q_9GtEbaCLBnUQ0W70OXsMPAnjthqNEPRwHjrSuunSdWEYpkc/s72-c/rsz_2373334_l-750x375.jpg
www.yanayojiri.com
http://nipasheapp.blogspot.com/2018/10/fahamu-mpangilio-wa-gia-kwenye-gari-ya.html
http://nipasheapp.blogspot.com/
http://nipasheapp.blogspot.com/
http://nipasheapp.blogspot.com/2018/10/fahamu-mpangilio-wa-gia-kwenye-gari-ya.html
true
3144336648072757917
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy
© Copyright www.yanayojiri.com | Designed By Me